Beka'a
Beka'a (pia: Beqaa, Biqâ na Becaa; kwa Kiarabu البقاع al-niqāʿ; ilijulikana siku za kale kama Coele-Syria) ni bonde lenye rutuba lililopo mashariki mwa Lebanoni kati ya safu za milima ya Lebanoni na milima ya Lebanoni ndogo .
Linaanza kaskazini, mpakani wa Syria, na kufuata urefu wote wa Lebanoni likielekea kusini. Urefu wake ni takriban kilomita 120 na upana wake 8-12 km. Mito muhimu ni Orontes (nahr al-asi) upande kaskazini na mto Litani upande wa kusini.
Kijiolojia ni sehemu ya kaskazini ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki likiendelea upande wa kusini katika bonde la mto Yordani.
Ni eneo muhimu zaidi kwa kilimo nchini Lebanon. Kuna kilimo cha mboga wa majani aina nyingi. Viwanda pia vipo vingi eneo hilo vinavyohusiana na kilimo.
Miji muhimu ni Zahlé na Baalbek.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Awali kipindi cha zama za chuma bonde la Beqaa kwa jumla lilikaliwa na Wafoinike - wakiongea na jamii na makabila. Bonde hilo lilikuwa kituo cha falme za Waarama katika karne ya 11. iligeuzwa kuwa kituo cha kabila na makabila ya Waarama, na kisha wakaanzisha mfumo wa usambazaji maji wa Damascus kwa kujenga mifereji na mahandaki ambayo yaliongeza ufanisi wa mto Barada.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Burns, Ross (2005). Damascus: A History. ISBN 978-0-415-27105-9.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Beka'a kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |