Jacob Zuma
Jacob Zuma | |
Rais wa Afrika Kusini (2009-2018)
| |
Deputy | Kgalema Motlanthe Cyril Ramaphosa |
---|---|
mtangulizi | Kgalema Motlanthe |
aliyemfuata | Cyril Ramaphosa |
Rais wa African National Congress (2007-2017)
| |
Deputy | Kgalema Motlanthe Cyril Ramaphosa |
mtangulizi | Thabo Mbeki |
aliyemfuata | Cyril Ramaphosa |
Makamu wa Rais wa Afrika Kusini (1999-2005)
| |
Rais | Thabo Mbeki |
mtangulizi | Thabo Mbeki |
aliyemfuata | Phumzile Mlambo-Ngcuka |
tarehe ya kuzaliwa | 12 Aprili 1942 Nkandla, Afrika Kusini |
chama | African National Congress |
ndoa | Gertrude Sizakele Khumalo (1973–) Kate Mantsho (1976–2000) Nkosazana Dlamini (1982–1998) Nompumelelo Ntuli (2008–) Thobeka Mabhija (2010–) Gloria Bongekile Ngema (2012–) |
watoto | 20 |
Jacob Gedleyihlekisa Zuma (* 12 Aprili 1942) alikuwa Rais wa Afrika Kusini tangu mwaka 2009 hadi 2018, alipojiuzulu.
Alikuwa makamu wa rais Thabo Mbeki kati ya 1999 na 2005.
Tangu Desemba 2007 hadi 2017 alikuwa mwenyekiti wa chama tawala cha ANC.
Kijana na mwanaharakati wa ANC
[hariri | hariri chanzo]Alikuwa mtoto wa wazazi maskini katika eneo la KwaZulu-Natal. Akiwa na umri wa miaka 17 akajiunga na ANC akaingia katika upinzani mkali dhidi ya serikali ya apartheid (ubaguzi wa rangi wa kisheria).
Mwaka 1963 alikamatwa akafungwa jela miaka 10 huko Robben Island pamoja na Nelson Mandela. Baada ya kuondoka gerezani akatoka Afrika Kusini akashiriki katika shughuli za nje za ANC huko Msumbiji na Zambia.
Aliingia katika uongozi hadi kuwa mkuu wa ujasusi wa jeshi la ANC.[1]
Kupanda ngazi katika Afrika Kusini huru
[hariri | hariri chanzo]Tangu ANC kuhalalishwa tena nchini Afrika Kusini mwaka 1990, Zuma alikuwa mwenyekiti wa chama cha Natal na baada ya uchaguzi wa 1994 akawa waziri katika serikali ya jimbo.
Mwaka 1997 alikuwa Makamu wa Mwenyekiti wa ANC na mwaka 1999 akateuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri.[2]
Kuachishwa kazi serikalini 2005
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2005 mshauri wake Shabir Shaik alihukumiwa miaka 15 jela kwa sababu alipokea rushwa. Zuma alishtakiwa pia na Rais Thabo Mbeki aliyemwachisha umakamu wa Rais. Kesi hii ilisimamishwa kwa sababu mashitaka hayakuandaliwa vizuri[3].
Miezi michache baadaye alishtakiwa tena kwa sababu mama mmoja alidai ya kuwa alinajisiwa na Zuma.[4] Katika kesi hii Zuma hakuhukumiwa kwa sababu hakimu aliamini madai kwamba mama yule alikubaliana naye.
Kurudi kwake kama kiongozi wa ANC 2007 na uraisi 2009-2018
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2007 Zuma akagombea nafasi ya mwenyekiti wa ANC dhidi ya Thabo Mbeki aliyetaka kuchaguliwa tena akamshinda.
Baada ya ushindi wa ANC kwenye mwaka 2009 bunge lilimchagua Zuma kuwa rais wa taifa. Alirudishwa kama mwenyekiti wa ANC mwaka 2012 na kuwa mgombea wa urais 2014.
Katika uchaguzi wa kitaifa ANC ilipotea kura ikirudi bungeni na asilimia 62 za kura zote. Zuma lichaguliwa upya kuwa rais.
Tangu 2016 upinzani dhidi yake iliongezeka. Ulisababishwa na mashtaka ya kuhusishwa na rushwa, uhusiano wake wa karibu sana na familia tajiri wa Gupta, na ugomvi ndani ya serikali yake baada ya kufukuza mara mbili waziri wa fedha kulikofuatwa na vurugu wa kiuchumi.
Tarehe 8 Agosti 2017 kulikuwa na kura ya siri bungeni ya kumwondoa Zuma madarakani iliyoshindwa ingawa safari hii pia idadi kubwa ya wabunge wa ANC walikubali.
Mwisho wa 2017 ulitokea tena mkutano mkuu wa ANC pamoja na uchaguzi wa uongozi mpya. Zuma alimtaka Nkosazana Dlamini-Zuma (aliyewahi kuolewa naye mnamo 1982 akipata talaka 1998) kwa nafasi ya mwenyekiti wa chama atakayegombea baadaye pia urais. Lakini mkutano ulimchagua kuwa kiongozi wa chama Cyril Ramaphosa, makamu wa rais aliyewahi kupinga sehemu za siasa ya Zuma na hasa uenezaji wa rushwa.
Katika Februari 2018 kamati kuu ya ANC chini ya uongozi wa Ramaphosa ilidai Zuma ajiuzulu. Baada ya kukataa kwa muda na kutishwa na kura ya kumwondoa madarakani hatimaye Jacob Zuma aliitikia akajiuzulu tarehe 14 Februari 2018.
Mnamo Septemba 2021, Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini ilitupilia mbali kwa nguvu ombi la Rais wa zamani Jacob Zuma la kubadilisha uamuzi wake uliomhukumu kifungo cha miezi 15 gerezani kwa kudharau haki.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Trials of Jacob Zuma, tovuti ya BBC, iliangaliwa Februari 2018
- ↑ Jacob Gedleyihlekisa Zuma, Return to South Africa, tovuti ya sahistory, iliangaliwa Februari 2018
- ↑ Deputy president sacked, gazeti la Rand and Mail ya 14 Juni 2005, iliangaliwa Februari 2018
- ↑ Zuma's rape accuser questioned, tovuti ya BBC ya 7 Machi 2006, iliangaliwa Februari 2018
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Profile at the African National Congress
- Zuma: Road to the presidency
- Jacob Zuma Archived 1 Septemba 2011 at the Wayback Machine. at Who's Who Southern Africa Archived 1 Septemba 2011 at the Wayback Machine.
- Jacob Zuma at the Internet Movie Database
- Shughuli au kuhusu Jacob Zuma katika maktaba ya WorldCat catalog
- Full text of the judgement Archived 12 Julai 2010 at the Wayback Machine. against Schabir Shaik, Zuma's financial advisor
- Supreme Court judgment upholding 2009 ruling