Nenda kwa yaliyomo

Jeradi Sagredo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Jeradi akimlea Mt. Emeriko wa Hungaria.

Jeradi Sagredo, O.S.B. (Venezia, Veneto, Italia, 23 Aprili 980 hivi - Budapest, Hungaria, 24 Septemba 1046) alikuwa mmonaki Mbenedikto aliyeinjilisha Hungaria chini ya mfalme wa kwanza, Stefano wa Hungaria, aliyemfanya askofu wa Csanad (10001038)[1].

Hatimaye aliuawa na Wapagani kwa kupigwa mawe, akaitwa Mtume wa Hungaria.

Papa Gregori VII alimtangaza mtakatifu tarehe 20 Agosti 1083 pamoja na Stefano na mwanae, Emeriko wa Hungaria, aliyelelewa naye.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.