Nenda kwa yaliyomo

Kidole cha shahada

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kidole cha shahada
Majina ya vidole vya mkono:
1 Kidole gumba, 2 Kidole cha shahada,
3 Kidole kirefu, 4 Kidole cha pete, 5 Kidole cha mwisho

Kidole cha shahada ni kidole cha pili mkononi. Iko kati ya kidole gumba na kidole kikubwa. Kidole hiki kinatumiwa sana kwa mawasiliano kati ya watu.

Kwanza hutumiwa kwa kukilenga kwa kitu kwa kwa mtu kwa kusudi la kumaanisha: Ndiye huyu, ndicho hiki! Pia kinadokeza mweleko au upande. Kwa lugha mbalimbali jina la kidole hiki ni "kidole cha kuonyesha" (kiing. index au pointer finger, kijer. Zeigefinger).

Matumizi mazuri hutegemea na utamaduni.

  • Kuna utamaduni mbalimbali ambako ni mwiko au tabia mbaya kukilenga kwa mtu.
  • Kama mkubwa anakitumia kwa wadogo ni kama onyo: "Usifanye tena hivyo!", "Si vizuri hivyo".
  • Kidole hiki kinatumiwa pia kuonyesha namba "1".
  • Kinaweza kumaanisha ushindi; katika Kenya alama ya kidole cha shahada kilitumiwa kama alama ya chama cha KANU.


Sehemu za Mkono wa binadamu

Bega * Mkono wa juu * Kisugudi * Kigasha * Kiganja * Kidole gumba * Kidole cha shahada * Kidole cha kati * Kidole cha pete * Kidole cha mwisho