Nenda kwa yaliyomo

Mariolojia ya Kiorthodoksi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mozaiki ya Theotokos, Ravenna, 560 hivi.

Mariolojia ya Kiorthodoksi haitegemei sana utafiti wa wanateolojia bali Heshima ya pekee kwa Bikira Maria inayotolewa kwake na waumini katika ibada kwa Mwenyezi Mungu aliyemuumba, hasa ya liturujia.

Kwa namna fulani heshima kwa bikira Maria inapenya maisha yote ya Makanisa ya Kiorthodoksi, kama "wanda" wa dogma na wa maisha ya kiroho sawia. Ingawa inafanana sana na ile ya Kanisa Katoliki, Mariolojia ya Waorthodoksi si fani ya pekee, bali ni sehemu tu ya Kristolojia na ya Eklesiolojia vilevile. [1]

Teolojia ya Kiorthodoksi inamuita Maria "Theotokos", yaani Mzazi wa Mungu. Umama wake wa Kibikira ndio kiini cha Mariolojia yake, inayomuita mfululizo "Bikira Daima". Pia inasisitiza utakatifu wa ajabu wa Maria, kushiriki kwake katika kazi ya Mwanae ya kuleta ukombozi na nafasi yake katika ugawaji wa neema[2][3]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mariolojia hiyo ina mizizi yake katika maandishi ya Mababu wa Kanisa, hasa wa Ukristo wa Mashariki, yaliyofikia kilele chake katika yale ya Yohane wa Damasko (karne ya 8)[4][5].

Katika karne ya 14, Mariolojia ya Kiorthodoksi ilistawishwa na wanateolojia wa Bizanti waliounganisha Yesu na Maria wakiwaweka pamoja kama kiini cha ulimwengu na kama lengo la historia yote.

Katika karne ya 20 Mariolojia hiyo ilipata msukumo mpya huko Urusi, ambapo Sergei Bulgakov na wengineo walianza kupanga kitaalamu sifa za Maria[6][7] [8], wakisisitiza uhusiano wake na Roho Mtakatifu.

  1. Schmemann, Alexander (1970) "On Mariology in Orthodoxy," Marian Library Studies: Vol. 2, Article 4, Pages 25-32. Available at: http://ecommons.udayton.edu/ml_studies/vol2/iss1/4
  2. .Rahner, Karl 2004 Encyclopedia of theology: a concise Sacramentum mundi ISBN 0-86012-006-6 pages 393-394.
  3. The encyclopedia of Christianity, Volume 3 by Erwin Fahlbusch, Geoffrey William Bromiley 2003 ISBN 90-04-12654-6 page 409.
  4. Damascene, John. Homily 2 on the Dormition 14; PG 96, 741 B.
  5. Damascene, John. Homily 2 on the Dormition 16; PG 96, 744 D.
  6. The Orthodox Church by Sergei Nikolaevich Bulgakov 1997 ISBN 0-88141-051-9 page 67.
  7. The Celebration of Faith: The Virgin Mary by Alexander Schmemann 2001 ISBN 0-88141-141-8 pages 60-61.
  8. Modern Russian Theology: Orthodox Theology In A New Key by Paul Vallierey 2000 ISBN 0-567-08755-7 pages.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mariolojia ya Kiorthodoksi kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.