Nenda kwa yaliyomo

Nyuki mkata-majani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyuki mkata-majani
Megachile lagopoda (angalia chavua kwenye tumbo)
Megachile lagopoda (angalia chavua kwenye tumbo)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Nusuoda: Apocrita (Hymenoptera wenye kiuno chembamba)
Familia ya juu: Apoidea
(bila tabaka): Anthophila
Familia: Megachilidae
Latreille, 1802
Jenasi: Megachile
Ngazi za chini

Spishi >100 katika Afrika ya Mashariki: Angalia matini

Nyuki wakata-majani (kutoka Kiing. leafcutter bees) ni nyuki wadogo hadi wakubwa sana wa jenasi Megachile ya family Megachilidae katika familia ya juu Apoidea ya oda Hymenoptera wanaokata vipande vya majani wanayotumia kupamba viota vyao. Hata hivyo, sio spishi zote za jenasi hii hukata majani. Baadhi hutumia sandarusi kufunga vijumba vya kizazi na kwa hivyo huitwa nyuki-sandarusi. Spishi za jenasi Trachusa vilevile hukata majani lakini hutumia sandarusi pia. Megachile ina spishi nyingi, zaidi ya 1500[1], zinazotokea duniani kote. Afrika ya Mashariki ina spishi takriban 100.

Ukubwa wa nyuki hawa ni mm 5-38. Megachile pluto ni nyuki mkubwa kabisa duniani. Mwili ni imara mwenye kichwa kikubwa. Mandibulo za majike zina meno 3 hadi 5. Tarsi hazina ndewe (arolio) kati ya kucha, kwa hivyo hawawezi kutembea kwenye nyuso laini kama glasi. Kutikulo ya spishi nyingi ni nyeusi isiyokolea, ingawa spishi nyingine hung'aa kama metali. Rangi zao hutoka kwa nywele, ambazo nyingi ni nyeupe au ya maziwa lakini zinaweza kuwa njano au nyekundu, au hazipo. Nywele zimepangwa kwa miraba kutoka upande mmoja wa mwili hadi upande mwingine na/au kandokando ya pande, na usoni. Kinyume na familia nyingine, familia ya nyuki wakata-majani hawana nywele maalum kwenye tibia ili kunasa na kushikilia chavua. Badala yake, wana nywele kama hizo kwenye tumbo lao. Inaitwa skopa (scopa).

Kama jina linavyoonyesha, nyuki hawa hukata vipande vya mviringo kutoka kwa majani, ambavyo huvitumia kupamba mashimo yao ya viota. Hata vipande vya karatasi ya plastiki vimepatikana[3]. Wanatafuna kingo ili kuunganisha vipande pamoja. Spishi nyingi za jenasi hii huenda hatua zaidi na kutafuna vipande vya majani kabisa hadi viwe rojo, ambayo huitumia kuunganisha mchanga, kokoto ndogo, vipande vya makoa ya konokono n.k. Sandarusi pia hutumiwa, pamoja na au bila rojo ya mimea. Katika miji, ambapo sandarusi inaweza kuwa vigumu kupata, nyuki mara nyingi pia huchukua kalafati sinasia kutoka majengo[4].

Spishi takriban zote hutumia mashimo yaliyopo kuweka viota vyao. Hayo yanaweza kuwa matawi yenye uwazi, mashimo katika miti, nyufa za miamba, mashimo kwenye majengo, mashimo ya viota ya zamani na hata makoa tupu ya konokono. Pia wanapokea kwa furaha "hoteli za nyuki" zinazotolewa na watu na kufanywa kutoka kwa mabua au vibomba vyenye uwazi, au magogo yaliyopekechwa mashimo ndani yao. Idadi fulani ya spishi huchimba mashimo yao yenyewe kwenye udongo tifutifu kiasi.

Viota vya nyuki wakata-majani huwa na safu ya vyumba vya kizazi, kila kimoja kikiwa kimefungwa kwa dutu ya ujenzi inayotumiwa na spishi fulani. Chavua, pengine pamoja na mbochi kulingana na spishi, huviringishwa katika tufe kwa msaada wa mate na kuwekwa katika kila chumba na yai hutagwa kwenye kila tufe. Buu anayeibuka huanza kujilisha kwa chavua na kupitia hatua nne kabla ya kuwa bundo. Hatua ya mwisho ya buu huchukua kipindi cha kupumzika ili kusubiri mwisho wa majira ya baridi au kiangazi. Hii inahakikisha kwamba mpevu anaibuka mwanzoni mwa msimu unaofaa, wakati maua yanachanua na chavua ni tele.

Majike hukusanya chavua na mbochi kutoka kwa maua ya ama spishi moja au chache au ya spishi nyingi kulingana na spishi ya nyuki. Kwa sababu ya ulimi wao ndefu wanaweza kuchagua aina kubwa za maua. Spishi fulani ni muhimu sana kwa uchavushaji wa mimea na miti, k.m. nyuki mkata-majani wa luseni, Megachile rotundata.

Spishi za Afrika ya Mashariki

[hariri | hariri chanzo]
  • Megachile accraensis
  • Megachile aculeata
  • Megachile admixta
  • Megachile altera
  • Megachile anomomaculata, nyuki-sandarusi
  • Megachile antinorii, nyuki-sandarusi
  • Megachile apiformis
  • Megachile armatipes
  • Megachile arnoldiella, nyuki-sandarusi
  • Megachile astridella
  • Megachile atroalbida
  • Megachile attenuata
  • Megachile battorensis
  • Megachile benitocola
  • Megachile bilobata, nyuki-sandarusi
  • Megachile bituberculata
  • Megachile bombiformis
  • Megachile boswendica
  • Megachile bucephala
  • Megachile capitata
  • Megachile caricina
  • Megachile catulus
  • Megachile chrysopogon
  • Megachile chrysorrhoea, nyuki-sandarusi
  • Megachile cincta
  • Megachile cognata
  • Megachile combinata
  • Megachile congruens
  • Megachile coniformis
  • Megachile conradsi
  • Megachile cradockensis
  • Megachile crassitarsis
  • Megachile curtula
  • Megachile dariensis
  • Megachile decemsignata
  • Megachile discolor
  • Megachile disjuncta, nyuki-sandarusi
  • Megachile dolichognatha
  • Megachile epixanthula
  • Megachile eupyrrha
  • Megachile eurymera
  • Megachile felina
  • Megachile filicornis
  • Megachile fimbriata
  • Megachile formosa, nyuki-mwashi (mason bee)
  • Megachile fulva
  • Megachile fulvitarsis
  • Megachile funebris
  • Megachile gastracantha
  • Megachile globiceps
  • Megachile gowdeyi
  • Megachile granulicauda
  • Megachile gratiosa
  • Megachile griseola
  • Megachile harrarensis
  • Megachile hecale
  • Megachile hemirhodura
  • Megachile hirticauda
  • Megachile ianthoptera
  • Megachile ikuthaensis
  • Megachile imperialis, nyuki-sandarusi
  • Megachile invenita, nyuki-sandarusi
  • Megachile janthopteriana
  • Megachile katonana
  • Megachile kigonserana
  • Megachile kimilolana
  • Megachile konowiana
  • Megachile laminata
  • Megachile leonum, nyuki-sandarusi
  • Megachile luteociliata
  • Megachile lydenburgiana
  • Megachile mabirensis
  • Megachile magadiensis
  • Megachile manyara
  • Megachile marshalli
  • Megachile masaiella
  • Megachile maxillosa
  • Megachile meruensis
  • Megachile montibia, nyuki-sandarusi
  • Megachile muansae
  • Megachile nasalis
  • Megachile neavei
  • Megachile nigroaurea
  • Megachile nigrocaudata
  • Megachile opaculina
  • Megachile persimilis
  • Megachile polychroma
  • Megachile postnigra
  • Megachile pseudolaminata
  • Megachile pyrrhothorax
  • Megachile riggenbachiana
  • Megachile rosarum
  • Megachile rufa
  • Megachile ruficheloides
  • Megachile rufigaster
  • Megachile rufipennis
  • Megachile rufipes, nyuki-sandarusi
  • Megachile rufiventris, nyuki-sandarusi
  • Megachile rufohirtula
  • Megachile rufoscopacaea
  • Megachile selenostoma
  • Megachile semierma
  • Megachile semivestita
  • Megachile silverlocki, nyuki-sandarusi
  • Megachile sinuata
  • Megachile tangensis
  • Megachile torrida, nyuki-sandarusi
  • Megachile transiens, nyuki-sandarusi
  • Megachile truncatipes, nyuki-sandarusi
  • Megachile umbiloensis
  • Megachile ungulata
  • Megachile utra, nyuki-sandarusi
  • Megachile venusta
  • Megachile venustella
  • Megachile vittatula
  • Megachile voiensis
  • Megachile zebrella
  • Trachusa eburneomaculata, nyuki mkata-majani anayetumia sandarusi pia
  • Trachusa flavorufula, nyuki mkata-majani anayetumia sandarusi pia
  1. Michener, Charles Duncan (2000). The Bees of the World. Baltimore: JHU Press. ku. 556.
  2. 2.0 2.1 https://idtools.org/id/bees/exotic/factsheet.php?name=16425
  3. Goldman, Jason G (Juni 1, 2014). "Bees Living in Cities Are Building Their Homes with Plastic". Scientific American. 310 (6). Iliwekwa mnamo 20 Septemba 2014.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "City bees line nests with plastic bags". University of Washington Conservation Magazine (Conservation This Week). Februari 13, 2014. Iliwekwa mnamo 5 Oktoba 2014.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)