Sundakuwili
Sundakuwili | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Sundakuwili mashariki (Eryx colubrinus)
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||
Spishi 12:
|
Sundakuwili ni spishi za nyoka wa jenasi Eryx katika familia Boidae. Wamepewa jina hili kwa sababu ncha zote mbili zinaonekana sawa.
Nyoka hawa ni wafupi. Spishi ndefu kabisa (E. conicus) inaweza kufika mita moja, lakini spishi fupi hufika sm 40 tu. Kichwa kina umbo wa risasi bila shingo na wenye macho madogo. Mkia ni mfupi, chini ya 10% ya urefu mzima. Kwa kawaida wana mabaka kahawia au meusi juu ya msingi wa rangi nyepesi kama kijivu, njano au machungwa, lakini kuna namna zilizo na rangi moja kama nyekundu, kahawia, hudhurungi au kijivu.
Sundakuwili hujificha chini ya mchanga au hukaa katika vishimo vya wanyama au chini ya mawe. Mawindo yakija karibu nyoka hushambulia kwa kasi kubwa. Mawindo ni wagugunaji na ndege wadogo, mijusi na nyoka wengine wadogo. Spishi nyingine huwinda mchana, nyingine usiku.
Kama chatu nyoka hawa hawana sumu na huua mawindo kwa ubinyaji. Huzongomeza mwili wao kuzunguka kidari cha mawindo kisha kubana kwa nguvu ili kuzuia mawindo asipumue mpaka akufe. Halafu humwakia mzima.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Eryx borrii, Sundakuwili Somali (Borri's sand boa)
- Eryx colubrinus, Sundakuwili Mashariki (Kenya sand boa)
- Eryx jaculus, Sundakuwili Kaskazi (Javelin sand boa)
- Eryx muelleri, Sundakuwili Magharibi (Müller's sand boa)
- Eryx somalicus, Sundakuwili wa Pembe Afrika (Somali sand boa)
Spishi za Asia na Ulaya
[hariri | hariri chanzo]- Eryx conicus (Rough-tailed sand boa)
- Eryx elegans (Central Asian sand boa)
- Eryx jayakari (Arabian sand boa)
- Eryx johnii (Red sand boa)
- Eryx miliaris (Dwarf sand boa)
- Eryx tataricus (Tartar sand boa)
- Eryx whitakeri (Whitaker's sand boa)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Sundakuwili magharibi
-
Rough-tailed sand boa
-
Arabian sand boa
-
Red sand boa
-
Dwarf sand boa
-
Tartar sand boa
-
Whitaker's sand boa
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sundakuwili kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |