Uchafuzi wa bahari
Uchafuzi wa bahari ni hali inayotokana na shughuli mbalimbali zinazohatarisha mazingira ya bahari.
Shughuli hizi mara nyingi hutokana na binadamu mwenyewe, katika hali ya kujitafutia riziki za kila siku, hususani katika kipindi hiki cha ukuaji wa teknolojia za viwanda, na mara nyingi huwa ni za uvuvi baharini pamoja na zile ambazo hufanyika karibu au pembezoni mwa bahari husika.
Bahari za dunia kwa karne nyingi zimeonekana kuwa sehemu mahususi za kutupia taka. Hivyo sasa imepelekea kwa wingi kiasi kikubwa cha uchafu kimezidi kuwa kingi sana, mpaka hupelekea athari katika bahari kuu kwa viumbe wanaoishi ndani yake.
Uchafuzi huu wa bahari kwa kiasi kikubwa huonekana katika fukwe za bahari kuu ambazo hupokea kila aina ya uchafu unaotokana na shughuli za binadamu.
Bahari kuu za dunia
[hariri | hariri chanzo]Bahari hizo ni kama vile:
Vyanzo vya uchafu baharini
[hariri | hariri chanzo]Vyanzo ambavyo mara nyingi huhusishwa na utupaji wa taka ni kama vile, mito iliyo na maji machafu ambayo huelekea baharini, kutokana na uchafuzi wa hali ya hewa ambao hupelekea bahari kuchafuka. Hivyo mito hii inayoelekea baharini mara nyingi hubeba vitu kama vile: maji taka, mbolea na sumu za wadudu, uchafu kutoka katika migodi, mashamba ya chumvi;taka za nyuklia, viwanda vya chuma, kampuni za karatasi, visima vya mafuta, usafirishwaji wa mafuta, viwanda vya kusindika vyakula.
Picha
[hariri | hariri chanzo]Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |